Watu waliopoteza makazi Sudan Kusini wafikia 121,600

Kusikiliza /

Wakimbizi wa Sudan Kusini waliofurushwa makwao

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na misaada ya kibinadamu OCHA, limesema kuwa kiasi cha watu 121,600 wamepoteza makazi huko Sudan Kusin kutokana na machafuko yaliyozuka mwezi disemba na kunauwezekano idadi hiyo ikaongezeka zaidi.Taarifa zaidi na Grace Kaneiya.

(Taarifa ya Grace)

Kiasi cha watu 63,000 wameomba hifadhi katika kambi za Umoja wa Mataifa zilizoko katika maeneo yaJuba, Bor, Malakal, Bentiu na Pariang. Huko Juba kwenyewe watu waliopoteza makazi wanakadiriwa kufikia  25,000.

Mashirika ya kimataifa ya kutoa misaada yanasema kuwa yameanza kusambaza huduma za dharura na jambo muhimu wakati huu ni kusambaza chakula, nguo,matibabu na huduma za majisafina salama.

Hata hivyo kutokana na ukosefu wa usalama mashirika ya misaada yameshindwa kupata nafasi ya kulifikia ghala lililoko Bor na kuna wasiwasi kuwa huenda vitu vilivyomo kwenye ghala hilovimeanza kuharibika.
Mashirika hayo yamesema kuwa ili kufanikisha kampeni yake ya utoaji huduma, yanahitaji msaada wa dola za Marekani milioni 166.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mwakilishi wa Katibu Mkuu na Mkuu wa UNMISS, Hilde Johnson alielezea mahitaji ya kibinadamu Sudan Kusini

"Kwa ujumla, imekadiriwa kuwa Sudan Kusini inahitaji hadi dola bilioni 1.1 za kufadhili misaada ya kibinadamu. Dila milioni 166 ni zile zinazohitajika kwa sasa. Tunaendelea kutoa huduma za chakula, makazi, maji, na nyingiezo kama za afya kwa raia walio kambini mwetu. Kuota huduma za kibinadamu sio jukumu la ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa, na hatuna uzoefu katika uwanja huo. Itakuwa bora ikiwa wadau wetu wa huduma za kibinadamu watayatekeleza majukumu hayo muhimu."

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031