Wananchi wa CAR wanakabiliwa na hali ngumu: OCHA

Kusikiliza /

Babacar Gaye, Mwakilishi maalum mpya wa Katibu Mkuu wa UM huko Jamhuri ya Afrika ya Kati

Mtu mmoja kati ya kila watu watano nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati ametoroka nyumbani kwake, huku ghasia mjini Bangui zikiwa zimesababisha zaidi ya watu 200,000 kuhama makwao mwezi huu wa Disemba pekee. Hayo yameibuka katika ripoti mpya ya Ofisi ya Kuratibu Missada ya Kibinadamu katika Umoja wa Mataifa, OCHA kuhusu hali ya huduma za kibinadamu kote duniani.

Katika mahojiano na Redio ya Umoja wa Mataifa, Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu na Mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo, MISCA, Babacar Gaye, amesema hali ya utulivu ilorejeshwa kwa muda wa miezi michache ilopita sasa umesambarika tena.

"Mara ya mwisho nilipozungumza na Radio ya UM, ilikuwa mara tu baada ya utulivu tuliokuwa tumerejesha kufuatia mzozo wa kisiasa, na nilisema matokeo hayo mazuri yalitupa matumaini, ingawa hali ilibakia kuwa tete. Sasa hali hiyo tete imethibitishwa, kwani sasa tumekuwa na kile tunachoweza kukiita Krismasi yenye matukio ya machafuko mjini, Bangui."

Bwana Gaye ameelezea zaidi ghasia ambazo zimeughubika mji mkuu wa Bangui

"Kumekuwa na ghasia, kwanza, dhidi ya askari ambao wameidhinishwa na Baraza la Usalama, ghasia miongoni mwa jamii, na ghasia baina ya makunid yenye silaha kutoka pande zote mbili ambazo zinalumbana mjini. Na, kwa bahati mbaya, hili limesababisha vifo vingi na mateso. Hali iliyopo inawafanya maafisa wengi wasifike kazini, kwani ni vigumu kuyafikia maeneo fulani ya makazi. Kwa hiyo, ni hali ngumu sana Bangui, ambayo MISCA na vikosi vya Sangari vinajaribu kutuliza."

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031