Waliokimbia mapigano huko Kamango wapatiwa hifadhi Uganda

Kusikiliza /

Wakimbizi wa DRC waliokimbilia nchini Uganda(picha ya faili)

Zaidi ya watu elfu moja na mia tano walioathiriwa na mapigano mjini Kamango mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) wamekimbilia nchi jirani ya Uganda. Ripoti kamili , na John Kibego wa redio washirika ya Spice FM, Uganda.

(Tarifa ya John Kibego)

Wakimbizi wanaeleza kuwa walitoroka mapigano makali kwenye mji wa mpakani wa Kamango, baina ya waasi na Jeshi la serikali ya DRC usiku wa kwamkia Krisimasi.

Maureen Mcbrien, Mratibu Mwandamizi wa shirika la Umoja wa Mataifa Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), kusini magharibi mwa Uganda amesema tayari wamefikisha wakimbizi 1400 hadi kambi ya muda ya Bubukwanga wilayani Bundibugyo kutoka eneo la mpakani.

(Sauti ya Maureen Mcbruen)

Kulingana na idadi ya jana, walikuwa elfu moja na mia nne, na mamia ya wengine walikuwa tayari wamevuka mpaka"

Wanapanga kuwamisha hadi kwenye kambi ya wakimbizi ya Kyangwali wilayani Hoima wiki ijayo.

Mashambulio yalipytowakimbiza makwao yanadaiwa kutekelezwa na waasi Uganda wa Allied Democratic Forces (ADF) waliokimbilia pori za DRC 1999 baada ya kuzidiwa nguvu na jeshi la serikali.

Sababu yao kushambulia waninchi na jeshi la serikali ya DRC, haieleweki.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Machi 2017
T N T K J M P
« feb    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
2728293031