Wahamiaji 18 raia wa Haiti waaangamia kwenye ajali baharini

Kusikiliza /

Nembo ya IOM

Karibu watu 18 wahamiaji raia wa Haiti wamezama baharini baada ya mashua waliyokuwa wakisafiria kuhusika kwenye ajali nje ya visiwa vya Turks na Caicos msimu huu wa Krismasi.

Kufuatia kutokea kwa ajali hiyo mkurugezni mkuu wa shirika la kimataifa la uhamiaji IOM William Swing ametuma rambi rambi zake na familia za waathirwa wa ajali hiyo akisema kuwa ni lazima zitafutwe njia za kupata chanzo kinachosababisha watu kusafirishwa kwa njia zilizo hatari.

Mashua hiyo ilizama ilipokuwa ikikaribia ardhi. Utawala wa visiwa vya Turks na Caicos uliwaokoa wahamiaji 32 na kupata miili yaw engine 18 umbali wa mita 150 kutoka ufuoni akiwemo mtoto wa kiume wa umri wa miaka 12.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Oktoba 2015
T N T K J M P
« sep    
 1234
567891011
12131415161718
19202122232425
262728293031