Viongozi CAR acheni kuchochea vurugu kwa misingi ya dini: Pillay

Kusikiliza /

Wakimbizi wanaokimbia ghasia CAR

Kamishna mkuu wa haki za binadamu ndani ya Umoja wa Mataifa Navi Pillay ametaka viongozi huko Jamhuri ya Afrika ya Kati kuacha kuchochea ghasia kwa misingi ya tofauti za kidini. Taarifa kamili na Jason Nyakundi.

(Taarifa ya JASON NYAKUNDI)

Pillay amesema kuwa yale yanayoendela yanashangaza na yanastahili kutoa ishara kote ulimwengu kuwa ikiwa hatua za haraka hazitachukuliwa huenda taifahilolikatumbukia kwenye janga. Anasema kuwa kundi la uchunguzi la Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika  yaKati imekuwa likinakili vitendo vya ukiukaji wa haki za binadamu ambavyo  vimeshuhudiwa siku za hivi majuzi yakiwemo mauaji, dhuluma za kimapenzi, kukamatwa, uvamizi hospitalini, uharibifu wa mali na kuwalenga watu kuambatana na misingi ya kidini.Ravina Shamdasani ni msemaji wa ofisi ya haki za binadamu ya UM

 (Sauti ya Ravina)

 "Kamishina mkuu alionya kuwa tofauti za kidini zilikuwa zinatumiwa na viongozi wa kisiasa zikiwa na matokeo hatari. Kwa kitu ambacho si cha kawaida tumeona kutumika kwa tofauti za kidini na kikabilka hali ambayo imesababisha madhara makubwa hasa ya kijamii kwa nchi.Nawataka viongozi wa kitaifa na kimaeneo kwenye Jamhuri ya Afrika ya kati kuacha kuchochea ghasia kwa misingi ya kikabila.Tumewaona vijana wa kiislamu wakichukua majukumu ya kulinda makanisa na makanisa yamekuwa mahala salama kwa wakimbizi wa ndani Hatua hizo ni za kutia moyo na ninatoa wito kwa viongozi wote wa kidini na kijamii kuweka juhudi zaidi kuhakikisha kuwa jamii hazijikuti kwenye ghasia ambazo tumekuwa tukizishuhudia."

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Machi 2017
T N T K J M P
« feb    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
2728293031