UNMISS yakaribisha kutengamaa kwa hali ya usalama Juba

Kusikiliza /

 

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, UNMISS umesema kuwa umeshuhudia hali kutengamaa kwa kiasi kikubwa mjini Juba leo, na hivyo kuruhusu wafanyakazi wake kuanza tena kutembea mjini asubuhi ya leo.

Taarifa kutoka UNMISS imesema ujumbe huo umeanza tena kuweka doria kwa kiwango kidogo mjini Juba, pamoja na kurejesha shughuli za usafiri wa ndege kwenda na kutoka Entebbe, Uganda. Taarifa hiyo pia imesema maisha katikati ya mji wa Juba yanarejelea hali ya kawaida. Hata hivyo, usalama wa raia katika mji huo mkuu wa Sudan Kusini bado ni suala la kuhofia, hususan katika vitongoji vilivyopo nje ya mji.

Mkuu wa UNMISS, Hilde Johnson ametoa wito kwa serikali ya Sudan Kusini kufanya kila iwezalo kumaliza ghasia zozote zinazoendelea, na kuhakikisha kuwa raia wanahisi tena kuwa salama kote mjini, nila kujali asili yao ya kikabila.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031