UNICEF na wadau waokoa maisha ya wakimbizi watoto huko Chad

Kusikiliza /

Watoto wakimbizi wa Sudan Kusini waliofurushwa makwao kufuatia mzozo unaoendelea

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF linaendelea na usaidizi wake kwa raia waliokimbilia Chad kutokana na machafuko yanyoendelea huko Jamhuri ya Afrika ya Kati na jimbo la Darfur nchini Sudan.  Taarifa zaidi na Grace Kaneiya

(Taarifa ya Grace)

Wakimbizi hao ni pamoja na watoto ambao wanakosa hakiyaoya msingi ya elimu pamoja na kuwa na msongo kutokana na yale waliyoshuhudia. Mshauri nasaha kutoka shirika la kiraia linalosaidiana na UNICEF kuokoa watoto Hassan Saleh Hassan anasema..

 (Sauti ya Hassan)

Mara kwa mara tunawauliza watoto kuhusu uzoefu wao. wanasema wameshuhudia miili ya watu iliyotelekezwa barabarani na mingine kwenye mashimo. Michezo tunayowapatia inawasaidia kusahau yale waliyoyaona."

Ili kufanikisha mustakhbali wa watoto, UNICEF na wadau wake wanaimarisha usaidizi kama anavyosema Bruno Maes, mwakilishi mkazi wa shirika hilo nchini CHAD.

 (Sauti ya Bruno)

“Wadau wote ikwemo UNICEF wanahakikisha hatua sahihi zinachukuliwa kusaidia watoto ambao ni sehemu ya wakimbizi wanaoingia Chad kutoka Jamhuri ya AFrika ya Kati na Darfur. Hiyo ni kuhakikisha haki zao za kuishi na elimu zinashughulikiwa kwa njia sahihi."

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031