UNFPA yatoa ripoti ya ubakaji mashariki mwa DRC miezi sita ya kwaza 2013

Kusikiliza /

Wanawake DRC

Jimboni Kivu ya kaskazini, zaidi ya vitendo vya ubakaji elfu tatu vilihesabiwa katika mitaa mbalimbali, katika kipindi cha miezi sita ya kwanza ya mwaka 2013.

Hayo yametangazwa katika ripoti ya wataalam wanao husika na ubakaji, kutoka wizara ya wanawake, shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na idadi ya watu, UNFPA, ujumbe wa Umoja wa Mataifa DRC, MONUSCO pamoja na mashirika mbalimbali yasiyo ya kiserikali.

Idadi hiyo ni mara mbili zaidi ya ile ya mwaka jana, na kwa wakati mmoja, katika mitaa ya Ruchuru, Lubero na Masisi, inaoathiriwa sana na ubakaji wa wanawake. Hali imetokana na ukosefu wa usalama katika maeneo yale, lakini hasa sana na kuwepo kwa makundi yenye silaha.

Kutoka Goma mshirika wetu Sifa Maguru wa Radio Okapi ana maelezo zaidi.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Febuari 2016
T N T K J M P
« jan    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
29