Umoja wa Mataifa wasikitishwa na ghasia Jahmhuri ya Afrika ya Kati

Kusikiliza /

Mtoto katika eneo moja lililoathirika kwa mapigano

Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na ujenzi wa amani katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, BINUCA, imeelezea masikitiko yake kufuatia matukio ya ghasia katika eneo la Boali, yapata kilomita 95 kutoka mji mkuu wa Bangui, ambapo raia wameuawa na wengine kujeruhiwa.

Watu wapatao 12 wameuawa, huku wengine 30 wakijeruhiwa, wakiwemo watoto kutokana na ghasia hizo ambazo zinafanywa kiholela na kunyanyapaliwa kwa jamii fulani.

Kufuatia kuendelea kuwepo mazingira ya machafuko katika CAR, BINUCA imetoa wito kwa mamlaka za mpito nchini humo kutimiza wajibu wao wa kuwalinda raia, na kuhakikisha walotekeleza vitendo hivyo vya ghasia wanawajibishwa kisheria, pamoja na kuendeleza utangamano wa kijamii nchini humo.

BINUCA pia imeelezea haja ya dharura ya kutekeleza vipengee vya azimio la Baraza la Usalama 2121, ambalo linawataka wafuasi wa Seleka kuweka chini silaha na kushiriki katika mipango ya kusalimisha silaha, kuvunja uasi na kurejea katika jamii.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Julai 2017
T N T K J M P
« jun    
 12
3456789
10111213141516
17181920212223
24252627282930
31