Umoja wa Mataifa waandaa mkakati wa kipaumbele kwa haki za binadamu

Kusikiliza /

Naibu Katibu Mkuu wa UM Jan Eliasson

Naibu Katibu Mkuu, Jan Eliasson, amewaambia waandishi wa habari mjini New York kuwa Umoja wa Mataifa umekuwa ukifanya kazi kuandaa mkakati wa kutoa kipaumbele kwa haki za binadamu, ambao utampa kila mmoja msukumo kufanya awezalo kuzuia ukiukwaji wa haki za binadamu, hususan katika mazingira ya migogoro. Bwana Eliasson ametaja mambo matatu muhimu ambayo mkakati huo unalenga kutimiza

"Kwanza ni kufanya uelezewa wa haki za binadamu uenee katika mfumo mzima wa Umoja wa Mataifa. Pili, bila shaka, ni ulinzi wa raia- tunazungumzia wakati huu. Kuwalinda raia huwa tatizo pale tunaposhindwa kuzichukulia dalili za mwanzoni za  ukiukwaji wa haki za binadamu kwa uzingativu kama tunavyopswa kufanya. Tatu ni suala la ndani kuhusu jinsi utaratibu wetu ulivyo na maandalizi yetu kukabiliana na hali ambazo zinazobadilika kuwa janga la halaiki."

Bwana Eliasson amesema mkakati huo umetokana na Mkataba Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Mkataba wa kimataifa kuhusu haki za binadamu, pamoja na matukio kama yale ya mauaji ya kimbari Rwanda mwaka 1994, na Srebrenica mwaka 1995.

Bwana Eliasson amehoji, ikiwa ukiukwaji wa haki za binadamu ni mwanzo wa jambo linaloweza kuwa janga la kibinadamu na kusababisha operesheni kuu kisiasa na katika ulinzi wa amani, ni kwa nini hatua zisichukuliwe pale ambapo tishio hilo la kuwa janga linapoanza kujitokeza?

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031