UM wataka uchunguzi dhidi ya ukiukaji haki unaofanywa na wawindaji Ivory Coast:

Kusikiliza /

Moja ya vikao vilivyoandaliwa na UNOCI kuelimisha wawindaji asili juu ya kuheshimu haki

Ripoti ya Umoja wa mataifa imetoa wito wa kufanyika uchunguzi dhidi ya ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu uliotekelezwa na wawindaji wa asili wajulikanao kama Dozos  kati ya mwezi Machi 2009 na Mei mwaka 2013 nchini Ivory Coast.

Ripoti hiyo iliyotolewa leo na mpango wa Umoja wa Mataifa nchini humo UNOCI kwa kushirikiana na ofisi ya kamishina mkuu wa haki za binadamu , inaelezea uhalifu mkubwa wa ukiukaji wa haki za binadamu uliofanywa na Dozos wakati wakifanya masuala ya usalama.

Uhalifu huo ni pamoja na kukiuka haki ya mtu kuishi, yakiwemo mauaji, unyongaji, kukamatwa kinyume cha sheria na kuwekwa rumande, uporaji na manyanyaso mengine.

Mathalani takribani watu 228 waliuawa, 164 walijeruhiwa kwa risasi, mapanga na visu na wengine 162 wakikamatwa na kushikiliwa kinyume cha sheria na wawindaji hao wa asili katika kipindi hicho.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Machi 2017
T N T K J M P
« feb    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
2728293031