Uganda yawaondoa raia wake na watu wengine Sudan Kusini

Kusikiliza /

Raia wa Uganda na nchi jirani watoroka ghasia zinazoshuhudiwa Sudan KUSINI

Wakati hali ikiwa bado ni tete nchini Sudan Kusini, nchi mbali mbali zinajitahidi kuwaondoa raia wao walio hatarini ili kuwaepusha na machafuko hayo yalioyoanza wiki moja ilopita. Serikai ya Uganda ilituma ndege za kijeshi huko Juba, na sasa msemaji wa jeshi hilo anasema wamefanikiwa kuwaokoa takriban raia 1,000 wa Uganda na raia wa nchi nyingine. John Kibego wa redio washirika ya Spice FM na ripoti kamili.

(RIPOTI YA JOHN KIBEGO)

Jeshi maalum la serikali ya Uganda liliingia mji mkuu wa nchi hiyo, Juba wiki iliyopita kwa madhumuni ya kuokoa raia wake waliokwama mapiganoni na kuulinda mji wa Juba, likiitikia wito wa Seikali ya Sudan Kusini.

Kujua zaidi kuhusu jitihada za jeshi hilo kuwatafuta na kuwarejesha nyumbani watu hao, nimeongea na Msemaji wa jeshi hilo Lt. Col. Paddy Ankunda.

(Mahojiano na Pady Ankunda)

Juhudi za jeshi la serikali ya Sudan Kusini kuyakomboa maeneo ya Bor na Bentiu yalioanguka mikononi mwa wapiganaji wa Riek Machar zinaendelea, huku Mratibu wa Umoja wa Mataifa wa maswala ya kibinaadamu nchini humo, Toby Lanzer akieleza kusikitishwa kwake na kiasi cha vurugu.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Oktoba 2017
T N T K J M P
« sep    
 1
2345678
9101112131415
16171819202122
23242526272829
3031