Pillay apongeza kuachiliwa kwa wafungwa wa kisiasa nchini Myanmar

Kusikiliza /

Navi Pillay

Kamishina mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Navi Pillay amepongeza hatua ya rais wa Myanmar Thein Sein ya kuwaachilia huru wafungwa wa kisiasa waliofungwa kwa makosa yakiwemo kukusanyika kinyume na seria na uhaini.

Pillay anasema kuwa hiyo ni hatua kubwa  na pia ni ishara ya maendeleo katika kutauza tatizo linalohusu wafungwa wa kisiasa nchini Myanmar.

Amesema kuwa lengo lao ni kushirikiana na serikali na washika dau wengine na kufanyia mabadiliko sheria ili kuhakikisha kuwa hakuna kesi zilizosalia zinazohusu wafungwa wa kisiasa.

Hata hivyo ameelezea kujutia kwake kutakana na kutoachiliwa kwa wafanyikazi watatu wa mashirika ya kimataifa ambao wamekuwa wakizuiliwa kwenye jela ya Buthidaung tangu mwezi  Juni mwaka 2012.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Oktoba 2017
T N T K J M P
« sep    
 1
2345678
9101112131415
16171819202122
23242526272829
3031