Nchi za Asia Pasifiki zapitisha azimio la kihistoria kuhusu ushirikiano wa kiuchumi

Kusikiliza /

ESCAP

Nchi za Asia-Pasifiki zimeridhia kwa kauli moja azimio la kihistoria linaloweka bayana mwelekeo wa kuwa na jumuiya ya kiuchumi ya kikanda. Azimio hilo limepitishwa katika mkutano wa ngazi ya mawaziri wa nchi wanachama wa Tume ya Umoja wa Mataifa kwenye ukanda huo, ESCAP, ambapo maafisa kutoka mataifa 36 waliridhia azimio laBangkokkuhusu ushirikiano wa kiuchumi na kikanda kwenye eneohilo.

Wameazimia kufanya kazi pamoja kujenga soko jumuishi linalounganisha shughuli za nishati, usafirishaji na fedha kwa lengo la kukabiliana na soko lisilo tulivu. Katibu Mtendaji wa ESCAP Dkt. Noleen Heyzer amesema kitendo hicho ni cha kihistoria kwa taasisi hiyo kwani kinatoa fursa kwa nchi wanachama kuimarisha na kupanua wigo wa ushirikiano bainayao. Amesema bila shaka azimiohilolinaweka bayana karne ya Asia Pasifiki.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2017
T N T K J M P
« jul    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031