Naibu Kamanda wa UNMISS azungumzia ujio wa vikosi vya nyongeza

Kusikiliza /

 

Askari walinda amani wa UNMISS

Naibu Kamanda Mkuu wa vikosi vya ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, UNMISS Brigedia Jenerali Asit Mistry amesema bado haijafahamika ni lini askari wa kuongeza nguvu kwenye kikosi hicho watawasili kufuatia azimio la Baraza la Usalama la kuongeza askari hao maradufu.

Akizungumza mjini Entebbe, Uganda akiwa njiani kuelekea Juba Brigedia Jenerali Mistry amesema suala muhimu wafike Sudan Kusini haraka iwezekanavyo, akitanabaisha kuwa hawawezi kuja wote kwa mpigo bali kwa makundi.

Baraza la usalama liliidhinisha askari  5,500 na polisi 440 na hivyo kuongeza idadi kuwa  takribani 14,000 kutoka 12,500 wa sasa.

Kwa mujibu wa UNMISS yawezekana nyongeza hiyo ikatoka kwenye vikosi vya Umoja wa Mataifa vinavyolinda amani DR Congo, Darfur, Abyei, Côte d'Ivoire na Liberia ili kusaidia mzozo huo Sudan Kusini uliosababisha mamia ya raia kuuawa na maelfu kukimbia makwao

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Mei 2017
T N T K J M P
« apr    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031