Mzee Nelson Mandela hakuwa mtu wa kujikuza: Naibu Mkuu UNAMA

Kusikiliza /

Nicholas Haysom, Naibu Mkuu wa UNAMA ambaye aliwahi kuwa Mshauri Mkuu wa masuala ya sheria wa Mzee Mandela

Nicholas Haysom, raia wa Afrika Kusini ambaye alifanya kazi ya Mshauri Mkuu wa masuala ya Sheria kwa Mzee Nelson Mandela wakati wa kipindi chake chote cha Urais na hata baada ya kustaafu wadhifa huo, amesema Madiba hakuwa mtu wa kujikuza.

Haysom ambaye kwa sasa ni Naibu Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchiniAfghanistan, amesema hayo kwenye mahojiano maalum kwa njia ya simu kutokaKabulna Ben Malor wa Radio ya Umoja wa Mataifa. Amesema Mzee Mandela alijiweka ngazi sawa na wale aliokuwa anafanya nao kazi hata kama walikuwa na umri mdogo kwake ambapo alitaja tukio muhimu analokumbuka.

(Sauti ya Haysom)

 Haysom akaenda mbali zaidi na kueleza sababu ya kwanini Mzee Mandela aliweza kusamehe na hata kuepuka visasi licha ya kuwa na kumbukumbu dhahiri ya yale aliyofanyiwa.

(Sauti ya Haysom)

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Oktoba 2017
T N T K J M P
« sep    
 1
2345678
9101112131415
16171819202122
23242526272829
3031