Mwakilishi wa UM Somalia alaani shambulio la Bossaso

Kusikiliza /

Mwakilishi wa UM, Somalia Nicholas kay

Mwakilishi maalumu wa UM nchini Somalia Nicholas Kay, amelaani vikali shambulio la kikatili dhidi ya majeshi ya serikali huko Puntland . Katika shambulio hilo la Jumatano alfajiri mshambuliaji wa kujitoa mhanga akiwa na mabomu kwenye gari alilenga vikosi vya serikali mjini Bossaso.

Kwa mujibu wa duru za habari mjini humo watu kadhaa wameuawa na wengine kujeruhiwa katika shambuliohilo. Puntland hivi sasa imo katikati ya mchakato wa uchaguzi ambao ni wa kupata bunge jipya huku ule wa Rais ukitarajiwa Januari 2014.

Bwana Kay amesema kitendo hicho cha woga hakina sababu yoyote na kwamba Umoja wa Msataifa unaendelea kusimama na watu wa Puntland wanapojitahidi kusaka utulivu na mustakhbali wa matumaini. Ametuma pia salamu za rambira, kwa wale waliopoteza ndugu na jamaa katika shambulio hilo na kuwatakia nafuu ya haraka waliojeruhiwa.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031