Mtaalamu wa UM aitaka Azerbaijan kuwalinda wanawake

Kusikiliza /

 

Rashida Manjoo

Mjumbe huru wa Umoja wa Mataifa Rashida Manjoo  leo ameitaka Azerbaijani kutekeleza kikamilifu sheria ya sasa na pia kuwachukuliwa hatua kali si wale tu waliohusika na vitendo vya unyanyasaji dhidi ya wanawake bali hata wale ambao walishindwa kuzuia vitendo hivyo.

Amesmea kuwa mamlaka za dola zinapaswa kuhakiisha kwamba vitendo vyote vya unyanyasaji dhidi ya wanawake vinaondoka na kwamba jambo hilo linapaswa kufanyika kwa kuzingatia sheria za kimataifa.

Mtaalamu huyo wa masuala ya haki za binadamu pia ameipongeza serikali kwa hatua zake za kuendeleza na kutetea haki za binadamu ikiwemo pia kuridhia sheria zinazozingatia usawa wa kweli.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Mei 2017
T N T K J M P
« apr    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031