Mtaalam wa UM wapongeza kuachiliwa kwa wafungwa Myanmar

Kusikiliza /

Tomás Ojea Quintana

Mtaalam huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya haki za binadamu nchini Myanmar, Tomás Ojea Quintana, amekaribisha kuachiwa huru kwa wafungwa 44 wa kisiasa nchini humo.

Mtaalam huyo huru amesema kuachiwa huru kwa wafungwa hao ni hatua muhimu katika kuona kuwa wafungwa wote wa kisiasa wameachiwa huru ifikapo mwishoni mwa mwaka huu. Ameongeza kuwa tangu mwaka 2008, kulikuwepo na wafungwa 1,900 wa kisiasa, lakini sasa idadi hiyo ni chini ya 50, na kuipongeza kazi ya kamati ya kurejelea na kutathmini kesi za wafungwa wa kisiasa.

Amesema anataraji kuwa kamati hiyo itaongezewa mamlaka ili iweze kufuatilia hali ya wafungwa hao wanaoachiliwa, akiongeza kuwa desturi ya kuwafunga watu kwa tofauti zao za dhana za kisiasa imekita mizizi katika miaka 50 ya uongozi wa kijeshi, na itachukuwa muda kufikia demokrasia, ambapo watu wanaruhusiwa kujieleza.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2017
T N T K J M P
« jul    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031