MONUSCO yachukua hatua kufuatia mapigano huko DRC

Kusikiliza /

 

Vikosi vya polisi na askari wa DRC katika doria huko Kinshasa kufuatia shambulio la tarehe 30/12/2013

Huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo hii leo kumeripotiwa mapigano kwenye mji mkuu Kinshasa, Lubumbashina Kindu kati ya jeshi la serikali na watu wasiofahamika waliokuwa wamejihami ambapo ujumbe wa umoja wa mataifa nchini humo, MONUSCO umechukua hatua kuhakikisha usalama kwa watendaji na vikosi vyake kwenye maeneo hayo.

Msemaji waUmoja wa Mataifa Martin Nesirky amewaambia waandishi wa habari mjini New York, kuwa wakati wa mapigano hayo kwenye uwanja wa ndege mjini Kinshasa, mfanyakazi mmoja wa Umoja huo ambaye ni raia wa DRC alijeruhiwa. Hata hivyo hali ya utulivu imerejea.

(Sauti ya Martin)

Ujumbe huo umeripoti kuwa utulivu umerejea Lubumbashi na Kindu ambapo vikosi vya MONUSCO vilivyopiga kambi kwenye uwanja wa ndege vilikabiliana na washambuliaji waliokuwa na silaha. Mpaka sasa utambulisho na lengo la washambuliaji hao haijafahamika."

 

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Aprili 2016
T N T K J M P
« mac    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
252627282930