MONUSCO yaanza operesheni ya kuyang'oa makundi yenye silaha DRC

Kusikiliza /

Walinda amani wa MONUSCO wapiga doria Pinga Kivu Kaskazini

Brigedi maalum ya kijeshi ya Ujumbe wa Kuweka Amani katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, MONUSCO ilianza jana operesheni dhidi ya wapiganaji wa FDLR katika eneo la Kalembe, umbali wa zaidi ya kilomita mia moja kaskazini ya Goma, mashariki mwa DRC. Hayo yametangazwa Jumanne na kamanda wa majeshi ya MONUSCO, Jenerali Dos Santos Cruz katika mazungumzo ya kipekee na redio Okapi ya Umoja wa Mataifa.

(SAUTI YA SANTOS)

Jenerali Dos Santos Cruz, amesema kwamba ni mpango mrefu wa operesheni za kukabiliana na makundi yenye silaha ya DRC na ya kimataifa katika eneo hilo.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Mei 2017
T N T K J M P
« apr    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031