MONUSCO kuinua ustawi wa raia DRC

Kusikiliza /

Wakazi wa Pinga Kivu Kaskazini wanauza bidhaa sokoni wakati hali ya kawaida ikirejea kufuatia ulinzi wa MONUSCO

Naibu Mwakilishi maalum wa ujumbe wa kuweka utulivu katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, MONUSCO, Moustapha Soumaré , ambaye pia ni Mratibu Mkazi wa masuala ya kibinadamu na Mkuu wa UNDP nchini humo, amehitimisha ziara yake ya siku mbili mjini Goma hapo jana Alhamisi.

Mwishoni mwa ziara hiyo, Bwana Soumaré  amesema, ziara hiyo ya ujumbe wa kibinadamu wa Umoja wa Mataifa na Benki ya Dunia mjini Goma ni ishara ya kujitoa kwa Umoja wa Mataifa kuendelea kujali maslahi ya watu wa mashariki ya DRC, na kutizama namna ya kuwasaidia kwa kuinua hali yao ya maisha.

Hapa alimweleza Sifa Maguru wa Radio washirika Okapi kuhusu wanachotarajia kutimiza  katika jimbo la Kivu ya kaskazini, mashariki mwa DRC

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031