Mfumo wa kuwapatia vijana mafunzo ndani ya ajira ni njia moja ya kukabiliana na ukosefu wa ajira:ILO

Kusikiliza /

Mafunzo ya kazi ndani ya kazi

Shirika la kazi duniani, ILO limesema ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana unaweza kupatiwa muarobaini, iwapo waajiri wataridhia kuboresha mfumo wa kuwapatia mafunzo ndani ya ajira vijana kama njia mojawapo ya kuboresha stadi zao na kuchangia katika maendeleo ya kampuni na mashirika.

Hayo  yameibuka kwenye warsha iliyoandaliwa barani Ulaya na ILO kuhusu mwelekeo na  uthabiti wa mafunzo ndani ya ajira kwa vijana na suluhu yake kwa ukosefu wa ajira miongoni mwa kundi hilo. ILO ikaeleza kuwa mifumo ya mafunzo ndani ya ajira kwa vijana au apprenticeship imekuwa mkombozi kwa hatma ya ajira kwa vijana hao.

Kwa mujibu wa takwimu za ILO barani Afrika mwaka 2012 pekee vijana wenye ujuzi milioni 75 wenye umri kati ya miaka 15 hadi 24 walikosa ajira. Je mfumo huu unatumika katika nchizo na unaweza kuleta ahueni kwa kupunguza ombwe la takwimu hizo?

(PCKG JARIDA)

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Machi 2017
T N T K J M P
« feb    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
2728293031