Matumizi ya silaha za kemikali yaliibainika kutumika Syria:Ripoti OPCW

Kusikiliza /

Timu ya wataalam wa uchunguzi ya OPCW

Mnamo mwezi Septemba, serikali ya Syria ilifanya tangazo ambalo lilikaribishwa na wengi, pale ilipokubali kuwa ilimiliki silaha za kemikali, na ilikuwa tayari kuziteketeza kwa kushirikiana na jamii ya kimataifa. Kufuatia tangazohilo, timu ya pamoja ya Umoja wa Mataifa na Shirika la Kupinga Silaha za Kemikali, OPCW, iliundwa ili kufuatilia na kusimamia uteketezaji wa silaha hizo za kemikali. Viwanda na vifaa vya kuteketeza silaha hizo ndivyo vilivyotangulia kuharibiwa.

Na mnamo mwezi Disemba, tume ya uchunguzi iloongozwa na Profesa Selstrom pia iliwasilisha kwa Katibu Mkuu ripoti ya uchunguzi wake katika madai ya awali ya matumizi ya silaha hizo za kemikali. Akiipokea ripoti hiyo, Ban alikuwa na haya ya kusema

 (Sauti ya Ban)

Hapo mwakani, mkutano wa kimataifa kuhusu Syriaunatazamiwa kufanyika nchini Uswisi, ili kutafuta suluhu kwa mzozo uliopo sasa na kuweka mustakhbali mpya wa taifa hilo.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Julai 2014
T N T K J M P
« jun    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031