Mapigano Sudan Kusini yazidi kusambaa: OCHA

Kusikiliza /

Watu wa Sudan Kusini watafuta hifadhi katika ofisi za UNMISS baaada ya mapigano kuzuka siku chache zilizopita

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu usaidizi wa kibinadamu, OCHA imesema mapigano yaliyoanza Juba tarehe 15 mwezi huu yanazidi kusambaa hususan kwenye jimbo la Jonglei ambako watu Elfu Thelathini na Wanne yakadiriwa wamepoteza makazi yao. Ripoti kamili ya George Njogopa. Taarifa zaidi na George Njogopa

(Ripoti ya George)

Ripoti zinasema kuwa zaidi ya raia 34,000 wameomba hifadhi katika kambi za Umoja wa Mataifa zilizokoJuba, Born a Bentiu.

Hadi sasa tayari kumefanyika tathmini za awali kuhusiana na misaada inayohitajika kupelekwa kwa waathirika hao ambao wanatajwa kuwa katika wakati mgumu.

Kwa upande mwingine, mashirika ya utoaji wa misaada ya kibinadamu yameanza kusambaza inayohitajika kwa haraka .

 Jens Learke ni msemaji wa OCHA ambalo ni shirika la Umoja wa Mataifa la misaada ya kibinadamu.

(Sauti ya Jens)

Wakati hali ya kibinadamu kwa wakimbizi waliosaka hifadhi kwenye vituo vya UNMISS imekua ikiendelea kupanuka, wabia wa usaidizi wa kibinadamu wamekuwa wakisaidia UNMISS kutoa usaidizi wa kiufundi na huduma nyinginezo kama maji, malazi, na huduma za dharura za afya kwa mujibu  wa  mamlaka za ujumbe huo. Tathmini zaidi kuhusu mengineyo imepangwa kufanyika leo”

Katika hatua nyingine, shirika la afya ulimwenguni WHO limesema kuwa hospitali ya kufundishia iliyoko mjini Juba imepokea kiasi cha wagonjwa 400 na nusuyao wakiwa wamejeruhiwa vibaya.

Tarik Jasarevic ni msemaji wa  WHO .

(Sauti ya Tarik)

 

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930