Malala Yousafzai ashinda tuzo ya heshima ya UM

Kusikiliza /

Malala Yousafzai

Mtoto Malala Yousafzai ambaye ni mwanaharakati wa haki ya elimu kwa mtoto wa Kike kutoka Pakistani, ni miongoni mwa washindi Sita wa tuzo ya heshima ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa kwa mwaka huu wa 2013.

Kamati ya uteuzi imesema Malala na washindi wengine wamepatiwa tuzo hiyo kutokana na mchango wao wa kipekee wa utetezi wa haki za binadamu.

Jina la Malala lilitanda kwenye vyombo vya habari baada ya kunusurika kuuawa na watalibani mwezi Oktoba mwaka 2012 kutokana na utetezi wake kwa mtoto wa kike kupata elimu nchini humo.

Malala na washindi wengine wakiwemo mahakama ya kikatiba ya Mexicona mtetezi wa kutokomezwa kwa utumwa nchini Mauritania Biram Dah Abeid, watakabidhiwa tuzo hiyo tarehe 10 mwezi huu kwenye hafla maalum mjiniNew York.

Tuzo ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imekuwa ikitolewa kila baada ya miaka mitano kuanzia mwaka 1968 ambapo miongoni mwa washindi rais wa zamani wa AFrika Kusini Nelson Mandela.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Febuari 2016
T N T K J M P
« jan    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
29