Magonjwa yatokanayo na wanyama yaongezeka kwa binadamu: FAO

Kusikiliza /

Mfugaji akilisha kuku. (FAO)

Mwelekeo wa milipuko ya magonjwa duniani unazidi kubadilika kila uchao kutokana na ongezeko la idadi ya watu, kupanuka kwa kilimo na hata jinsi ya usambazaji wa chakula duniani, limesema shirika la kilimo cha chakula duniani FAO.

Ripoti ya shirikahiloiliyotolewa Jumatatu imesema kutokana na hali hiyo inatakiwa mpango wa pamoja wa kudhibiti tishio la magonjwa hayo yatokanayo na wanyama na binadamu kwani asilimia 70 ya magonjwa yaliyoibuka miongo ya karibuni yametoka kwa wanyama hasa pale binadamu anapohaha kupata mlo utokanao na wanyama.

Nchi zinazoendelea ziko hatarini zaidi kutokana na mwingiliano wa magonjwa ya binadamu na wanyama na kusema inatishia usalama wa chakula. Msaidizi wa Mkurugenzi Mkuu wa FAO kuhusu masuala ya kilimo na ulinzi wa watumiaji, Ren Wang anasema ripoti hiyo inadhihirisha umuhimu wa kushughulikia pamoja afya ya binadamu na ile ya wanyama na mazingira kwa ujumla katika kuchambua chanzo cha magonjwa.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Machi 2017
T N T K J M P
« feb    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
2728293031