Lishe bora itolewayo na WFP yaboresha afya ya wanaoishi na virusi vya HIV

Kusikiliza /

Mfanyakazi wa WFP akiendesha semina huko Jamhuri ya Dominica kuhusu lishe kwa watu wenye virusi vya HIV

Mlo sahihi na lishe bora humwezesha mtu anayeishi na virusi vinavyosababisha Ukimwi, HIV kuwa na afya bora na hata kuimarisha matibabuyaokwa kuendelea na matumizi ya dawa ya kukabiliana na magonjwa nyemelezi.

Ni ujumbe wa Mkurugenzi Mkuu wa shirika la mpango wa chakula duniani, WFP Ertharin Cousin, katika siku ya Ukimwi duniani tarehe Mosi Disemba, likirejelea mpango wake wa utoaji wa lishe kwa wenye HIV na Kifua Kikuu.

Amesema mwaka 2012 pekee, shirikalakeilisaidiazaidi ya watu Milioni Moja nukta Tano kwenye nchi 33 duniani kupitia mpango huo. Ametaja nchi za Afrika kusini mwa jangwa laSaharakuwa na idadi kubwa zaidi ya watu wanaoishi na HIV ambapo hata wakianza dawa kutokana na lishe duni Theluthi Moja wanashindwa kuendelea.

Bi. Cousin amesema kupitia mpango wa lishe bora kwa wenye HIV na Kifua Kikuu, WFP inasema imeweza kuwafikia watu zaidi ya Laki Nne nchini Zimbabwe, Laki Mbili nchini Msumbiji na Laki Tatu na Elfu Sabini na Tano nchini Ethiopia.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031