Ladsous azuru mashariki ya DRC

Kusikiliza /

Herve Ladsous ziarani DRC

Mkuu wa Operesheni za Ulinzi wa Amani katika Umoja wa Mataifa, Herve Ladsous, leo amezuru mji wa Pinga, kaskazini magharibi mwa mji wa Goma katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC, akiambatana na Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu na Mkuu ujumbe wa kuweka utulivu nchini humo, MONUSCO, Martin Kobler.

Akizungumza na waandishi wa habari, Bwana Ladsous amesema ziara hiyo imeashiria juhudi za MONUSCO za kuendelea kurejesha utulivu katika eneo hilo, kufuatia kuondoka kwa waasi na makundi mengine yenye silaha.

(SAUTI YA LADSOUS)

Hivi sasa MONUSCO imepeleka wahudumu wake wa kiraia pamoja na vikosi vya kijeshi huko Pinga.

Bwana Ladsous amesisitiza umuhimu wa kurejesha mamlaka ya kitaifa kwenye eneo hilo na huduma nyingine, pamoja na utekelezaji wa programu inayoongozwa na serikali ya upokonyaji silaha, uvunjaji uasi na kuwaingiza tena wafuasi wa makundi ya zamani yenye silaha katika jamii.

(SAUTI YA LADSOUS)

Hapo jana, Bwana Ladsous alikutana na Rais Joseph Kabila mjini Goma kujadili masuala muhimu yanayohusiana uimarishaji wa amani na utulivu mashariki mwa DRC, na msaada wa MONUSCO kwa serikali.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031