Kenya wasema Mzee Mandela hakuna wa kulinganishwa naye

Kusikiliza /

Mzee Mandela alipotembelea Kenya mara tu baada ya kutoka gerezani

Nchini Kenya Rais Uhuru Kenyatta na wananchi wake wametoa salamu kwa Taifa la Afrika Kusini, familia na wananchi kufuatia kifo cha Mzee Nelson Mandela, na hiyo ni katika salamu za rambirambi na maoni yao kama anavyoripoti mwandishi wetu wa Nairobi, Jason Nyakundi.

(Ripoti ya Jason)

Kifo cha Mzee Mandela kimegusa wengi siyo tu Afrika Kusini wala Afrika nzima bali pia ulimwengu wote. Marais mbali mbali wametuma salamu za rambirambi kwa kifo cha Mzee Mandela ambaye alisaidia nchi yake kuondoka katika minyororo ya ubaguzi. Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ni miongoni mwa marais hao na alikuwa na haya ya kusema..

 

 

Kwa niaba ya serikal na wananchi wa Kenya na kwa niaba angu binfasi napenda kutuma risala za rambirambi kwa wananchi wa Afrika Kusini, serikali, marafiki na familia ya Mzee Nelson Mandela. Nina ujumbe wa majonzi kwa Rais Jacob Zuma na mama Graca Machel. Tuko pamoja katika huzuni ya kumpoteza ambaye pengo lake haliwezi kuzibika."

Raia waKenyawana lipi la kusema?

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930