Kampeni dhidi ya baa la nzige Madagascar yazaa matunda

Kusikiliza /

Nzige, Madagascar

Kampeni ya kukabiliana na kuenea kwa tatizo la nzige nchini Madagascar imeanza kuzaa matunda huku juhudi za kutokomeza kabisa tatizo hilo zikiimarishwa. Kufanikiwa kwa kampeni hiyo kulikotishia uhai wa mavuno ya mahindi kutazamia kusadia usalama kwa chakula kwa mamilioni ya raia.Ripoti zaidi na Joseph Msami.

(Ripoti ya Msami)

Kampeni hiyo iliyotekelezwa kwa ushirikiano wa pamoja kati ya shirika la chakula na kilimo FAO na serikali yaMadagascar ni ya miaka mitatu kwa ajili ya kutokomeza kabisa tatizo na nzige.

Awamu ya kwanza ya kampeni hiyo ambayo inaelezwa kuanza kuzaa matunda inatazamiwa kukamilika ifikakpo mwaka 2016. Mratibu wa kampeni hiyo kutoka FAO Said Lagnaoui,amesema kuwa njia mbalimbali zinatumika ili kufanikisha agenda yake. Njia mbadala zinazotumika kuwadhibiti nzige hao ni pamoja na ile inayotumika kwa njia ya helkopta na ile na magari.

Kumekuwa na uangalifu mkubwa wa utumiaji madawa ili kuepuka athari zozote za kimazingira.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2017
T N T K J M P
« jul    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031