IOM yatoa ombi la dola milioni 13 kushughuliia mahitaji wa raia wa Ethiopia wanorejea nyumbani kutoka Saudi Arabia.

Kusikiliza /

IOM yasaidia waEthipia kurudi nyumbani

Shirika la kimtaifa la uhamiaji IOM limetoa ombi la dola milioni 13.1 kuweza kushughulikia mahitaji ya karibu wahamiaji 120,000 raia wa Ethiopia  wanaorejea nyumbani  kutoka nchini Saudi Arabia huku idadi ya wahamiaji wanaorejea nyumbani ikizidi kuongezeka .

Hadi jana Alhamisi zaidi ya wahamiaji 100,000 walikuwa wamepokelewa na serikali ya Ethiopia. Kati ya hao IOM ilitoa usaidizi wa moja kwa moja kwa zaidi ya watu 90,000. Karibu wahamiaji 7000 wanawasili kila siku.

Fedha hizo zinatarajiwa kufadhili huduma zinazotolewa na IOM zikiwemo za usafiri, huduma za kwanza na za kisakolojia, chakula , maji , makao ya muda kwa wahamiaji wanaowasili usiku pamoja na makao na usafiri kwa watoto wasio na wazazi.

IOM pia inagawa viatu na bidhaa zisizokuwa chakula kwa wahamiaji wengine.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Febuari 2016
T N T K J M P
« jan    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
29