ICC yasema Mandela hakutaka ukiukwaji wa haki

Kusikiliza /

ICC

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC huko The Hague, imeungana na watu wa Afrika ya Kusini, bara la Afrika na jumuiya ya kimataifa kuombeleza kifo cha jabali wa Afrika, Mzee Nelson Mandela aliyekuwa sauti ya usawa na haki.

ICC imesema ni wakati utawala wa Mandela mnamo Julai 17 mwaka 1998 nchi ya Afrika ya Kusini ikawa miongoni mwa mataifa 10 ya mwanzo kutia saini mkataba wa Roma kuhusu mahakama hiyo.

Mandela alisema bara la Afrika limeteseka vya kutosha na ukiukaji wa haki za binadamu na vyombo kama ICC vingekuwepo labda mateso hayo yasingekuwepo.

 

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Aprili 2017
T N T K J M P
« mac    
 12
3456789
10111213141516
17181920212223
24252627282930