Hali Sudan Kusini yaendelea kuwa tete

Kusikiliza /

Wahamiaji wanaotafuta hifadhi katika ofisi ya UNMIS kufautia jaribio la kupindua serikali, Sudan kusini

Wakati hali mjini Juba ikiripotiwa kutengamaa, raia wengi bado wanaripotiwa kutafuta hifadhi salama. Kufuatia ripoti ambazo bado hazijathibitishwa za wanfunzi kadhaa kuuawa katika Chuo Kikuu cha Juba, mamia kadhaa ya wanafunzi wengine walosalia kwenye chuo hicho, wameomba kupewa ulinzi kutoka kwa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa Sudan Kusini, UNMISS.

Katika eneo jingine mjini Juba liitwalo Ketor, takriban watu  2,000 hadi 5,000 wamekimbilia huko kutafuta usalama, na kuomba ulinzi pia kutoka kwa UNMISS

Hali Jonglei pia imeripotiwa kuzorota zaidi, na kule Akobo, inaripotiwa kuwa vijana wa kabila la Luo Nuer walikivamia kituo cha muda cha UNMISS ambako raia kadhaa wamekusanyika. Katika mkutano na waandishi wa habari Naibu Katibu Mkuu, Jan Eliasson amelaani shambulizi hilo

 

"Kituo chetu Jonglei kivamiwa, na tuna ripoti za watu kupoteza maisha- hatuna habari kamili bado- na Katibu Mkuu nami tunalaani uvamizi huo vikali. Nakaribisha ripoti za asubuhi ya leo kuwa Rais Salvar Kiir ana utashi wa kuingia mazungumzo ya amani, na kukemea wale kwenye upande wa Machar wanaotaka serikali kupinduliwa. Tuna ripoti kutoka upande huo pia za utashi wa kufanya mazungumzo. Huu ni mzozo wa kisiasa, na unahitaji kwa dharura kusuluhishwa kwa mazungumzo ya kisiasa"

 

UNMISS imesema itajaribu kuwaondoa wafanyakazi wake wasio na silaha Aboko, na kupeleka huko wanajeshi 60 zaidi kutoka Malakal hapo kesho.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Oktoba 2017
T N T K J M P
« sep    
 1
2345678
9101112131415
16171819202122
23242526272829
3031