Hali Sudan Kusini bado yayumbayumba

Kusikiliza /

Hilde Johnson

Hali nchini Sudan Kusini bado ni tete, zaidi ya wiki moja tangu kuanza mapigano yalofuatia kile kilichotajwa kuwa jaribio la kuipindua serikali ya Rais Salvar Kiir, ambaye amesema yu tayari kufanya mazungumzo ya amani bila masharti.

Tarere 24 mwezi huu, Baraza la Usalama lilipitisha azimio la kuidhinisha kuongeza vikosi vya kulinda amani kwa wanajeshi wengine 5,500, ingawa Naibu Kamanda wa UNMISS amesema haijulikani watawasili lini.

Hii leo, Mwakilishi wa Katibu Mkuu na Mkuu wa UNMISS, Hilde Johnson, amewahutubia waandishi wa habari haba kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa kwa njia ya video kutoka mji wa Juba

Hilde Johnson

"Siku kumi na moja zilizopita, umekuwa wakati mgumu sana kwa Sudan Kusini na raia wa taiafa hili changa. Matukio ya wiki ilopita yameibua jinamizi la miaka ilopita. Taifa ambalo limejengwa kwa miongo ya vita na migogoro lipo mashakani. Kwetu sisi, kilicho muhimu zaidi ni kutokomeza jinamizi hilo. Natoa wito kwa viongozi wa kisiasa Sudan Kusini kuamrisha vikosi vyao kuweka chini silaha na kutoa fursa kwa amani, na wafanye hivyo haraka."

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Febuari 2016
T N T K J M P
« jan    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
29