FAO yaonya uwezekano wa kujitokeza njaa Jamhuri ya Afrika ya Kati

Kusikiliza /

Moja ya kambi za muda huko Jamhuri ya Afrika ya Kati. Wakulima wanaoishi kwenye kambi kama hizi hawawezi kuendeleza shughuli za kilimo.

Pamoja na hali ya ukosefu wa usalama inayoendelea sasa huko Jamhuri ya Afrika ya Kati, hata hivyo wakulima wanaendesha juhudi katika msimu wa kilimo ili kujiepusha na baa la kutumbukia kwenye tatizo la njaa..

Tangu mwaka uliopita pale walipolazimika kukimbia mapigano, wakulima hao walilazimika kuyaacha mashamba yao na baadaye kuhamishia shughuli za kilimo kwenye misitu mikubwa .

Hali hiyo iliwafanya wakulima wengi kuwa na uzalishaji mdogo ikilinganishwa na msimu uliopita ambapo kutokana na mavuno mazuri waliyoyapata wameweza kuwa na hifadhi hadi katika kipindi cha mwezi February.

Hata hivyo shirika la chakula na kilimo FAO limeonya juu ya uwezekano wa kujitokeza kwa tatizo kubwa la njaa kama hali ya ukosefu wa usalama itaendelea hata kipindi cha kilimo.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930