Elimu kwa watoto nchini Syria yazidi kudorora: UM na wadau

Kusikiliza /

Watoto wa Syria, elimu yao sasa imekumbwa na sintofahamu kutokana na mzozo

Shirika la umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto ,UNICEF Kwa kushirikiana na shirika la kimataifa la kuhudumia watoto, Save the children, World Vision na shirika la Umoja wa Mataifa la wakimbizizi UNHCR wamezindua ripoti hii leo inayohusu mkwamo wa kielimu unaowakumba watoto wa Syria kutokana na mgogoro. Taarifa zaidi na Grace Kaneiya

(Ripoti ya Grace)

 

Ripoti hiyo inaonyesha kuwa tangu mwaka 2011 karibu watoto milioni 3 kutoka  Syria wamelazimika kuacha masomo kutokana na kuenea kwa mapigano ambayo yamesababisha kuharibiwa kwa shule na kuwaacha watoto wakiwa na hofu kubwa ya kurudi tena shuleni.

 

Ikiwa ni ya kwanza kuangazia masomo yalivyoathiriwa tangu kuanza kwa mzozo mwaka 2011 ripoti hiyo inasema mamilioni ya watoto wamekosa elimu , shule na  kuwapoteza walimu. Wengi wa watoto wamelazimika kuacha masomo ili kuzisaidia familia zo kutafuta kipato. Marixie Mercado ni msemaji wa UNICEF.

(Sauti ya Marixie)

Ndani mwaSyriamoja kati ya shule tano haziwezi kutumika  kwa kuwa zimeharibiwa kabisa au kwa sasa zinawahifadhi wakimbizi wa ndani.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930