Baraza la Usalama laelezea hofu kuhusu hali Sudan Kusini

Kusikiliza /

Wajumbe wa Baraza la Usalama wakinyoosha mkono kupiga kura

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeelezea kusikitishwa na kuibuka kwa machafuko nchini Sudan Kusini, kufuatia kinachoelezwa kuwa jaribio la kuipindua serikali ya Rais Salvar Kiir.

Akizungumza na waandishi wa habari Jumanne jioni mjini New York, rais wa Baraza hilo kwa mwezi huu, Balozi Gerard Araud wa Ufaransa, amesema

"Tunatiwa hofu sana, siyo tu kwa sababu ya kuibuka ghasia, bali pia kuwa idadi kubwa ya watu wanaoripotiwa kuuawa, hata ingawa kwa wakati huu idadi kamili haijathibitishwa, lakini tunajua ni kubwa. Pia tunafahamu mapigano hayo ni kwa misingi ya kikabila, na hivyo yanaweza kuitumbukiza nchi hiyo katika hali mbaya zaidi kwa ujumla. Kulingana na hali itakavyokuwa, tutaandaa mkutano mwingine wa Baraza la Usalama kuhusu Sudan Kusini."

Baraza hilo awali lilikuwa limekutana kujadili masuala yanayohusiana na ofisi ya Umoja wa Mataifa Afrika Magharibi, hususan diplomasia ya kuzuia mizozo, kusaidia harakati za amani na utekelezaji wa mkakati wa eneo la Sahel.

Inaelezwa kuwa takriban raia 13,000 wamekimbilia ofisi za Umoja wa Mataifa, UNMISS kutafuta usalama, ingawa maelezo yaliyopo sasa yanaonyesha mapigano hayo hayajawalenga raia moja kwa moja.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Febuari 2016
T N T K J M P
« jan    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
29