Ban azungumzia kuhitimishwa kwa mahakama maalum ya Sierra Leone

Kusikiliza /

Jengo la mahakama maalum kwa Sierra Leone

Hatimaye mahakama maalum kuhusuSierra Leoneimehitimisha kazi zake tarehe 31 Disemba baada ya miaka Kumi na moja ya utendaji wake. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amepongeza majaji, mahakimu na watendaji wote nchini humo na wale wa kigeni kwa mafanikio makubwa alosema yamepatikana kutokana na uwepo wake. Amesema Umoja wa Mataifa unajivunia ubia wake na serikali yaSierra Leonekatika kuanzisha mahakama hiyo malum ambayo ilihakikisha kuwepo kwa haki kwa uhalifu wowote uliotendeka wakati wa muongo mmoja wa mapigano ya wenyewe kwa wenyewe. Bwana Ban amesema ni wazi mahakama hiyo itakumbukwa kwa kuanzisha zama za uwajibikaji na kwamba haki ni jambo lisilo na mbadala kwa amani ya kudumu kwenye nchi baada ya mizozo.Kuanzia tarehe Mosi Januari mwaka 2014, mahakama maalum ndani ya Sierra Leone itachukua wajibu wa mahakama ya awali ili kuhitimisha majukumu yaliyokuwa yamebakia.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031