Ban asikitishwa na machafuko Sudan Kusini

Kusikiliza /

Katibu Mkuu wa UM, Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, ameelezea kusikitishwa na ripoti zinazoendelea kuibuka za machafuko yanayoendelea kusambaa katika maeneo mengi ya Sudan Kusini, ukiukwaji wa haki za binadamu na mauaji yanayochochewa na chuki za kikabila.

Katika taarifa ilotolewa na msemaji wake, Bwana Ban ameitaka serikali na makundi ya upinzani kuheshimu haki za raia na kuhakikisha usalama wao. Amewakumbusha kuhusu majukumu yao na uwajibikaji chini ya sheria ya kimataifa ya kibinadamu.

Katibu Mkuu pia amesema ujumbe wa Umoja wa Mataifa Sudan Kusini, UNMISS unafanya kila liwezekanalo katika hali hiyo ngumu ili kuwalinda raia na wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa na wa kimataifa walioko huko.

Ban ameshangazwa hasa na shambulizi lililofanywa dhidi ya kituo cha UNMISS Akobo, ambako raia walikuwa wametafuta usalama, na kwamba huenda raia wameuawa. Amesema ikiwa ni kweli, walofanya uhalifu huo ni lazima wakabiliwe kisheria.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031