Ban amteua Philippe Lazzarini wa Switzerland kuwa mwakilishi wa masuala ya misaada ya kiutu Somalia

Kusikiliza /

Philippe Lazzarini

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon leo ametangaza uteuzi wa Bwana Philippe Lazzarini wa Switzerland kuwa kaimu mwakilishi maalum mkazi na mratibu wa misaada ya kiutu nchini Somalia.

Kwa mujbu wa taarifa ilioyotolewa na ofisi ya msemaji wa katibu mkuu, Bwana Lazzarin ana uzoefu mkuu katika masuala ya usaidizi wa kiutu na uratibu wa kimataifa katika migogoro na maeneno ambayo yameondokana na migogoro kama Somalia ambako amekuwa mkazi na maratibu wa masuala ya kiutu na mwakilishi wa shirika la Umoja wa Mataifa la mendeleo UNDP tangu mwezi Mechi mwaka 2013.

Mteule huyo ameshika nyadhifa mbalimbali katika ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya kibinadamu, OCHA, na ana shahada ya masuala ya uchumi .

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2017
T N T K J M P
« jul    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031