Ban akaribisha makubaliano ya kusitisha mapigano Sudan Kusini na kuteuliwa wapatanishi wa IGAD

Kusikiliza /

Katibu Mkuu Ban Ki-moon ameongea na wanahabari kuhusu Sudan Kusini

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, amekaribisha makubaliano ya kusitisha mapigano Sudan Kusini, pamoja na kuteuliwa kwa timu ya wapatanishi katika mzozo uliopo nchini humo, kufuatia mkutano wa viongozi wa IGAD mjini Nairobi, Kenya hapo jana, Disemba 27.

Katika mkutano huo pia ilikubaliwa kuwa wafungwa wa kisiasa waachiwe huru, kama njia ya kujenga mazingira ya mazungumzo ya amani.

Bwana Ban ameipongeza IGAD kwa kazi yake na kusema kuwa yu tayari kuunga mkono kikamilifu harakati hizo, akiongeza kuwa Umoja wa Mataifa unasimama bega kwa began a watu wa Sudan Kusini, na utaendelea kufanya kila uwezalo ili kuwalinda raia walio hatarini na kutoa misaada muhimu ya kibinadamu.

Amesema ghasia zote, mashambulizi na ukiukwaji wa haki za binadamu ni lazima vikomeshwe mara moja, na kuwakumbusha wanaoutekeleza uhalifu huo kuwa watakabiliwa kisheria. Ametoa wito kwa serikali na wahusika wote katika mzozo huo kuhakikisha kuwa wanalinda haki na usalama wa raia.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031