Bahama yatakiwa kuwa na mkakati wa kitaifa wa kupambana na usafirishaji wa binadamu

Kusikiliza /

Joy Ngozi Ezeilo

Mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu usafirishaji wa binadamu Joy Ngozi Ezeilo ameitaka jumuiya ya Commonwealth ya Bahama kuendeleza na kutekeleza haraka mpango wa kitaifa wa haki za binadamu na unaozingatia waathirika ukilenga kupinga ukuaji wa usafirishaji wa binadamu.

 

Akiongea baada ya kufanya ziara nchini humo Bi Ezeilo amesema Bahama imedhihirisha utayari wa kukabiliana na biashra haramu ya binadamu na kuongeza kuwa hii inafuatiwa na hatua ya kuridhia mikataba ya kimataifa ihisuyo usafirishji haramu wa binadamu na sheria ya mwaka 2008 inayopiga marufuku uisafirishaji wa binadamu katika nyanja zote kwa wanaume, wanawake na watoto.

Hata hivyo mtaalamu huyo huru amesema nchi hiyo inakosa makakati madhubuti wa kitaifa wa kupambana na biashara haramu ya usafirishaji wa binadamu kwa kuweka malengo na majukumu ya kutekeleza mkakati wa kisheria huku ikijumuisha haki za binadamu na mbinu mbadala za kulinda waathirika wa matukio hayo.

Bi Ezeilo anatarajiwa kuwasilisha ripoti yake na mapendekezo kwa baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa mwezi June mwaka 2014.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Aprili 2017
T N T K J M P
« mac    
 12
3456789
10111213141516
17181920212223
24252627282930