Azimio kuhusu Jamhuri ya Afrika ya Kati limekuja wakati muafaka: Ban

Kusikiliza /

Maisha ya wananchi wa CAR ni ya kuhamahama kutokana na mizozo

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amekaribisha kitendo cha Baraza la Usalama kupitisha azimio namba 2127 linaloidhinisha kupelekwa kwa vikosi vya Umoja wa Afrika na vile vya Ufaransa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Katika taarifa, Bwana Ban amekaririwa akisema uamuzi huo umekuja wakati muafaka na kwamba unatuma ujumbe wa azma ya jamii ya kimataifa ya kupatia suluhu mzozo unaoendelea nchini humo.

Katibu Mkuu amesema ni vyema azimiohilokwa kasi ya aina yake ili wakazi wa nchi hiyo waepushwe na machungu yaliyodumu kwa muda sasa.

Halikadhalika amerejelea kauli kuwa Umoja wa mataifa uko tayari kuchukua hatua zozote muhimu kuhakikisha azimiohilolinatekelezwa. Wakati huo huo Katibu Mkuu amesema anatiwa hofu na kuendelea kuzorota kwa usalama kwenye mji mkuuBangui na viunga vyake na kutaka mamlaka husika kuchukua hatua kudhibiti vitendo hivyo.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Machi 2017
T N T K J M P
« feb    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
2728293031