Angalau hakuna mapigano kwa sasa mjini Bangui: UM

Kusikiliza /

Raia wakiwa wamesaka hifadhi kwenye uwanja wa ndege Bangui

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa huko Jamhuri ya Afrika ya Kati, Babacar Gaye amezungumzia hali halisi ya usalama nchini humo akielezea kuwa angalau sasa hakuna mapigano mji mkuu Bangui na kwamba kazi ya kupokonya silaha inaendelea. Akizungumza katika mahojiano kwa njia ya simu na Radio ya Umoja wa Mataifa kutoka mjini humo, Bwana Gaye amesema hata hivyo bado hawajaweza kuwapokonya silaha kundi kubwa la Seleka lakini kuna matumaini..

(Sauti ya Gaye)

“Ninaweza kusema kwamba hali inaaimarika ni kitu ambacho kitabadilika sidhani jana katikati ya mzozo tulipata njia ya kuelekea kutatua mzozo. Waziri Mkuu, Rais na Msemaji wa bunge walifanya mkutano na baadaye wakawahutubua wanahabari jambo ambalo lilipokelewa vizuri na wananchi.”

Mwakilishi huyo amesema Umoja wa Mataifa unazidi kujiimarisha viungani hususan nje ya mji mkuu, na suala la walinzi wa watoto na wanawake linazingatiwa wakati huu ambapo bado kuna wakimbizi wa ndani wapatao Elfu Themanini karibu na uwanja wa ndege na Bossangoa.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Machi 2017
T N T K J M P
« feb    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
2728293031