Nyumbani » 26/12/2013 Entries posted on “Disemba 26th, 2013”

Raia Ufilipino wahaha kutafuta makazi baada ya kimbunga

Kusikiliza / Ufilipino

Baada ya kimbunga Haiyan kuikumba Ufilipino na kuathiri mamilioni ya watu, sasa maeneo ya uma ndio hutumiwa na baadhi ya raia kujihifadi baada ya nyumba zao kuharibiwa vibaya na kimbunga hicho. K imbunga hicho kimkesababisha adha kadhaa kwa makundi ya watu kama anavyosimulia Grace Kaniya katika ripoti ifuatayo

26/12/2013 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban azidi kulaani kuongezeka kwa mapigano Syria

Kusikiliza / Watoto nchini Syria maisha yao yako hatarini

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon ameelezea kusononeshwa kwake na mapigano yanayozidi kuongezeka nchini Syria hususani Aleppo ambapo ripoti zinasema raia ni miongoni mwa mamia ya watu waliouwawa na kujeruhiwa. Taarifa iliyotolewa na msemaji wa ofisi ya Katibu Mkuu alhamisi mjini New York, inaeleza kuwa Katibu Mkuu Ban amelaani kile alichokiita kuongezeka [...]

26/12/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

MONUSCO yasaidia vikosi vya serikali ya DRC kuwango'a waasi wa ADF

Kusikiliza / Askari wa kulinda amani wa MONUSCO akiwa kwenye doria huko Kivu Kaskazini. (Picha-MONUSCO)

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, MONUSCO, umesema waasi kutoka kundi la Allied Democratic Forces, ADF kutoka Uganda walivamia ngome za jeshi la kitaifa la DRC, FARDC katika aneo la Beni na Kamango, mkoa wa Kivu ya Kaskazini, na kuzidhibiti ngome hizo kwa muda. Wakati wa uvamizi huo, waasi hao [...]

26/12/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Wananchi wa CAR wanakabiliwa na hali ngumu: OCHA

Kusikiliza / Babacar Gaye, Mwakilishi maalum mpya wa Katibu Mkuu wa UM huko Jamhuri ya Afrika ya Kati

Mtu mmoja kati ya kila watu watano nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati ametoroka nyumbani kwake, huku ghasia mjini Bangui zikiwa zimesababisha zaidi ya watu 200,000 kuhama makwao mwezi huu wa Disemba pekee. Hayo yameibuka katika ripoti mpya ya Ofisi ya Kuratibu Missada ya Kibinadamu katika Umoja wa Mataifa, OCHA kuhusu hali ya huduma za [...]

26/12/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UNMISS yaunga mkono juhudi za kikanda za kurejesha amani Sudan Kusini

Kusikiliza / wakimbizi wa ndani Sudan Kusini

Mwakilishi wa Katibu Mkuu na Mkuu wa ujumbe wa UNMISS, Hilde Johnson, amewahutubia waandishi wa habari kwa njia ya video leo na kusema kuwa taifa la Sudan Kusini limetumbukia katika hali ya sintofahamu na kuyumbayumba, na kutoa wito kwa viongozi kuchukua hatua za dharura kurejesha utulivu. Bi Johsnon ambaye amezuru kambi za watu walolazimika kuhama [...]

26/12/2013 | Jamii: Habari za wiki, Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Wataalamu huru wa UM walaani mashambulizi ya anga huko Yemen

Kusikiliza / Drones

  Wataalamu huru wa Umoja wa Matiafa kuhusu haki za binadamu leo wameelezea wasiwasi wao kufuatia shambulio la anga lililofanywa hivi maajuzi na ndege zisizo na rubani huko Yemen na kusababisha maafa kwa raia. Yadaiwa kuwa mashambulizi yanayotumia ndege hizo zinazoweza kusababisha maafa yalifanywa na vikosi vya Marekani. Kulingana na maafisa wa usalama raia 16 [...]

26/12/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Hali Sudan Kusini bado yayumbayumba

Kusikiliza / Hilde Johnson

Hali nchini Sudan Kusini bado ni tete, zaidi ya wiki moja tangu kuanza mapigano yalofuatia kile kilichotajwa kuwa jaribio la kuipindua serikali ya Rais Salvar Kiir, ambaye amesema yu tayari kufanya mazungumzo ya amani bila masharti. Tarere 24 mwezi huu, Baraza la Usalama lilipitisha azimio la kuidhinisha kuongeza vikosi vya kulinda amani kwa wanajeshi wengine [...]

26/12/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Watoto 31 wazaliwa nchini Sudani Kusini katika kambi ya UNMISS

Kusikiliza / Mama na mwanawe na askari wa UNMISS, mmoja wa watoto waliozaliwa Sudan Kusini siku kuu ya Krismasi

  Licha ya madhila ya mapigano wanayokumbana nayo raia wa nchi hiyo, wakati wa krismasi watoto 31 walizaliwa katika kliniki inayohudumiwa na ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo UNMISS mjini Juba . Hatua hiyo iliiibua furaha kwa  wauguzi kama meja Nour Sarin  (Sauti) “Ndiyo ninafuraha sana leo. Nimezalisha watoto wa kike watatu katika hospitali [...]

26/12/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wahamiaji 18 raia wa Haiti waaangamia kwenye ajali baharini

Kusikiliza / Nembo ya IOM

Karibu watu 18 wahamiaji raia wa Haiti wamezama baharini baada ya mashua waliyokuwa wakisafiria kuhusika kwenye ajali nje ya visiwa vya Turks na Caicos msimu huu wa Krismasi. Kufuatia kutokea kwa ajali hiyo mkurugezni mkuu wa shirika la kimataifa la uhamiaji IOM William Swing ametuma rambi rambi zake na familia za waathirwa wa ajali hiyo akisema [...]

26/12/2013 | Jamii: Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Somalia kamilisha mipango kuhusu haki za binadamu: Mtaalamu UM

Kusikiliza / Shamsul Bari

Mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masuala ya hali ya haki za binadamu nchini Somalia Shamsul Bari hii leo ameitaka serikali ya Somalia kukamilisha na pia kutekelza mpango wa amani kuhusu haki za binadamu uliozinduliwa na baraza la mawaziri mwezi Agosti. Taarifa zaidi na Jason Nyakundi. (Taarifa ya Jason) Bwana Bari amesema kuwa [...]

26/12/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNICEF yasaka mabilioni ya dola kuwanusuru watoto Syria

Kusikiliza / Watoto wa Syria

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na watoto UNICEF linahitaji dola Milioni 835 kwa mwaka ujao ili kufanikisha mpango wa utoaji misaada ya dharura kwa mamia ya watoto walioathirika na mapigano nchini Syria. Taarifa zaidi na Assumpta Massoi. (Ripoti ya Assumpta) Kiasi hicho ni ongezeko la asilimia 77 ikilinganishwa na ombi la mwaka uliopita, lakini [...]

26/12/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Naibu Kamanda wa UNMISS azungumzia ujio wa vikosi vya nyongeza

Kusikiliza / Askari walinda amani wa UNMISS

  Naibu Kamanda Mkuu wa vikosi vya ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, UNMISS Brigedia Jenerali Asit Mistry amesema bado haijafahamika ni lini askari wa kuongeza nguvu kwenye kikosi hicho watawasili kufuatia azimio la Baraza la Usalama la kuongeza askari hao maradufu. Akizungumza mjini Entebbe, Uganda akiwa njiani kuelekea Juba Brigedia Jenerali Mistry [...]

26/12/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Dola Milioni 116 zahitajika kunusuru maisha ya wananchi Sudan Kusini

Kusikiliza / Waathiriwa wa ghasia Sudan Kusini

  Huku mgogoro wa kivita ukiendelea kutokota Sudan Kusin, mashirika ya kutoa misaada ya kiutu yanasema kuwa yanahitaji kiasi cha dola za Marekani milioni 116 katika kipindi cha sasa hadi mwezi Mechi mwakani ili kuwawezesha watu walioathirika na machafuko hayo kurejea kwenye hali zao za kawaida.Mahitaji muhimu yanayohiyajika sasa ni pamoja na kuandaa mpango wa [...]

26/12/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031