Nyumbani » 24/12/2013 Entries posted on “Disemba 24th, 2013”

Baraza la Usalama lapitisha azimio la kuongeza vikosi vya amani Sudan Kusini

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-Moon katika kikao cha Baraza la Usalama kuhusu Sudan Kusini

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, leo limepitisha azimio la kuongeza vikosi vya walinda amani wa UNMISS nchini Sudan Kusini, kufuatia ombi la Katibu Mkuu kwamba idadi ya vikosi hivyo iongezwe ili kuimarisha utoaji wa ulinzi kwa raia na huduma za kibinadamu, chini ya kipengee cha 7 cha Mkataba wa Umoja wa Mataifa. Barazahilolimeamua [...]

24/12/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wataalam wa Umoja wa Mataifa wasikitikia ghasia kuenea na kuwalenga raia Sudan Kusini

Kusikiliza / DPKOIDPS

Washauri maalum wa Umoja wa Mataifa wameelezea hofu yao kuhusu kulengwa kwa raia katika mapigano  ambayo yameanza kufuata mkondo wa ghasia za kikabila nchini Sudan Kusini. Wahauri hao wa Katibu Mkuu ambao ni Adama Dieng anayehusika na kuzuia mauaji ya kimbari, Jennifer Welsh anayehusika na wajibu wa kulinda, wameonya kuwa mashambulizi yanayowalenga raia na wafanyakazi [...]

24/12/2013 | Jamii: Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Hatuondoki Sudan Kusini licha ya changamoto za kiusalama: Bi. Johnson

Kusikiliza / Hilde Johnson, Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa UM nchini Sudan Kusini na Mkuu wa UNMISS

Hatutaondoka Sudan Kusini,  tupo hapa na tutaendelea kujiimarisha kwa maslahi ya wananchi, ni kauli ya Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, Hilde Johnson alipozungumza na waandishi wa habari mjini Juba, ikiwa ni zaidi ya wiki moja tangu mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yaanze nchini humo. Amesema wameshuhudia kupanuka kwa [...]

24/12/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la usalama kukutana leo kujadili kuimarisha UNMISS

Kusikiliza / Baraza la Usalama

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, Hilde Johnson, leo amekuwa na mkutano na waandishi wa habari mjini Juba kuelezea hali halisi hivi sasa wakati ambapo raia Elfu 81 wamepoteza makazi yao tangu kuanza kwa mzozo huo zaidi ya wiki moja. Hayo yamefanyika wakati Baraza la Usalama likitarajiwa kukutana baadaye [...]

24/12/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

China yapiga hatua kuwaendeleza wanawake, lakini bado inakabiliwa na changamoto

Kusikiliza / Nembo ya Umoja wa Mataifa

Jopo la wataalamu wa Umoja wa Mataifa wanaohusika utokomezaji wa mifumo yote inayowakandamiza na kuwabagua wanawake limesifu namna Chinailivyopiga hatua kuendeleza ustawi wa wanawake, lakini hata hivyo limesema kuwa  bado kuna mengi yanapaswa kufanywa. Grace Kaneiya na taarifa kamili  (TAARIFA YA GRACE) Limesema kuna hali ya kusua sua juu ya utekelezaji kwa vitendo baadhi ya [...]

24/12/2013 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Pillay ataka pande zinazopigana Sudan Kusini kujali maisha ya raia

Kusikiliza / Navi Pillay

Kamishna wa Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa Navi Pillay amezitaka mamlaka zinazohusika katika mzozo wa Sudan Kusini kujiepusha na matumizi zaidi ya nguvu katika wakati ambapo taarifa zinasema kuwa mamia ya raia wameathiriwa zaidi baada ya mapigano hayo kuingia siku ya kumi. Pillay amesema binafsi imeingia na wasiwasi mkubwa kutokana na [...]

24/12/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wataalamu waeleza kutoridhika na mbinu za uchunguzi dhidi ya watuhumiwa wa ugaidi

Kusikiliza / Juan Mendez

Wataalamu wawili huru wa masuala ya kibidamamu wa Umoja wa Mataifa hii leo wamekaribisha kuchapishwa kwa ripoti ambayo ni uchunguzi  unaohusu mateso na ukiukaji mwingine wa haki za binadamu uliofanywa na uingereza dhidi ya watu wanaozuiliwa nchi za ng'ambo kwa minajili ya vita dhidi ya ugaidi. Hata hivyo mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa anayehusika [...]

24/12/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Zaidi ya raia 81,000 Sudan Kusini wamekosa makazi-OCHA

Kusikiliza / Waathiriwa wa ghaisa waliokimbia makwao na kusaka hifadhi UNMISS

Idadi ya watu waliopoteza makazi huko Sudani Kusini kutokana na machafuko yanayoendelea inakadiriwa kufikia jumla 81,000, lakini hata hivyo kuna uwezekano mkubwa wa idadi hiyo ikaongezeka. Wakati hali ya upatikanaji wa misaada ya kiutu kwa raia zaidi ya 45,000 ambao wameomba hifadhi katika kambi ya Umoja wa Mataifa siyo ya kuridhisha kutokana na kukosekana kwa [...]

24/12/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNHCR yachukua hatua za kusaidia wale waliohama makwao kwenye Jamhuri ya Afrika ya Kati

Kusikiliza / Wananachi wa CAR waliofurushwa makwao wasaka hifadhi katika Kanisa mji mkuu, Bangui

Huku makabiliano ya kijamii yakiendelea sehemu kadha za Jamhuri ya Afrika ya kati, shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR  lina wasi wasi mkubwa kuhusu masuala ya usalama pamoja na ya kibinadamu kwenye maeneo yanayowahifadhi idadi kubwa ya watu waliohama makwao. Taarifa zaidi na Assumpta Massoi.  (Taarifa ya Assumpta) Zaidi ya watu 710,000 [...]

24/12/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WFP yasambazia msaada wa chakula raia Sudan Kusini

Kusikiliza / WFP yatoa mgao wa chakula kwa waathiriwa wa ghasia Sudan Kusini

Shirika la mpango wa chakula duniani, WFP linasambaza chakula kwa raia wa Sudan Kusini waliokimbia ghasia zinazoendelea nchini humo kwa zaidi ya wiki moja sasa. Taarifa zinasema kuwa mgao huo ulianza Jumapili kwa wananchi Elfu Thelathini waliosaka hifadhi kwenye ofisi za ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, UNMISS huko Juba na Bentiu. WFP [...]

24/12/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031