Nyumbani » 23/12/2013 Entries posted on “Disemba 23rd, 2013”

Mapigano, mafuriko vyatatiza maisha ya raia Somalia

Kusikiliza / somalia-floods

Wakati macho na masikio ya jumuiya ya kimataifa yakielekezwa nchini Sudan Kusini ambako kuna mapigano ya kikabila, nchi nyingine iliyoko pembe yaAfrika,Somalianayo inakabiliana na changamoto ya mapigano ya kikabila. Mapigano hayo yamesababisha hali mbaya kwa raia ambao wameshindwa kufikiwa na  misaada ya kibinadamu kutokana na mafuriko kukumba eneo ambako makabila hayo yanapigana liitwalo Johwar. Ungana [...]

23/12/2013 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Nimejizatiti kuimarisha uwezo wa UNMISS katika kulinda raia Sudan Kusini: Ban

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon ameongea na wanahabari kuhusu Sudan Kusini

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amezungumza na waandishi wa habari mjini New York hii leo kuhusu mzozo wa kikabila unaoendelea nchini Sudan Kusini na kusema kuwa leo anaendelea na jitihada za kuhakikisha kuwa raia nchini humo wanalindwa. Ametaja hatua hizo kuwa ni pamoja na kulishirikisha baraza la usalama. (Sauti ya Ban) "Karibu [...]

23/12/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Nchi za Asia Pasifiki zapitisha azimio la kihistoria kuhusu ushirikiano wa kiuchumi

Kusikiliza / ESCAP

Nchi za Asia-Pasifiki zimeridhia kwa kauli moja azimio la kihistoria linaloweka bayana mwelekeo wa kuwa na jumuiya ya kiuchumi ya kikanda. Azimio hilo limepitishwa katika mkutano wa ngazi ya mawaziri wa nchi wanachama wa Tume ya Umoja wa Mataifa kwenye ukanda huo, ESCAP, ambapo maafisa kutoka mataifa 36 waliridhia azimio laBangkokkuhusu ushirikiano wa kiuchumi na [...]

23/12/2013 | Jamii: Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Mashirika ya UM yazindua mpango wa kuokoa chakula

Kusikiliza / Mradi huo wa miaka mitatu utalenga kupunguza uharibifu wa chakula

Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanayohusika na chakula yamezindua mpango wa pamoja wenye shabaha ya kukabiliana na tatizo la upotevu wa chakula duniani. George Njogopa na taarifa zaidi. (Taarifa ya George) Yote kwa pamoja, mashirika hayo lile la mpango wa chakula duniani WFP, Shirika la chakula na kilimo FAO na fuko la kimataifa la maendeleo [...]

23/12/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban awateua Kufour na Stolternberg kumsaidia masuala ya mabadiliko ya tabianchi

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-Moon na John Agyekum Kufuor (Maktaba)

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon leo ametangaza kuwateuwa wajumbe wawili ambao watawajibika katika eneo la mabadiliko ya tabia nchi. Walioteuliwa ni rais mstaafu wa Ghana John Kufuor na waziri mkuu wa zamani wa Norway Jens Stoltenberg. Ban amewataka wajumbe hao kuzunguka duniani kote na kuwa na majadiliano na viongozi wa kiserikali ili [...]

23/12/2013 | Jamii: Habari za wiki, Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Zimbabwe yaandaliwa mradi wa kuendeleza kilimo

Kusikiliza / Mkulima, Zimbabwe

Shirika la misaada la Uingereza, DFID kwa kushirikiana na shirika la chakula na kilimo FAO yameanzisha mpango wa pamoja wa miaka minne kwa ajili ya kuisaidia Zimbabwe kukabiliana na tatizo la chakula kwa familia maskini. Grace na taarifa zaidi. (Grace Taarifa) Mpango huo ambao unakusudia kubainisha chanzo cha umaskini pamoja na tatizo la ukosefu wa [...]

23/12/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Uganda yawaondoa raia wake na watu wengine Sudan Kusini

Kusikiliza / Raia wa Uganda na nchi jirani watoroka ghasia zinazoshuhudiwa Sudan KUSINI

Wakati hali ikiwa bado ni tete nchini Sudan Kusini, nchi mbali mbali zinajitahidi kuwaondoa raia wao walio hatarini ili kuwaepusha na machafuko hayo yalioyoanza wiki moja ilopita. Serikai ya Uganda ilituma ndege za kijeshi huko Juba, na sasa msemaji wa jeshi hilo anasema wamefanikiwa kuwaokoa takriban raia 1,000 wa Uganda na raia wa nchi nyingine. [...]

23/12/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Misaada yawafikia maelfu watu walioathiriwa na ghasia nchini Sudan kusini

Kusikiliza / Misaada imewafikia waathiriwa wa ghasia, Sudan Kusini

Mashirika ya utoaji misaada yamechukua hatua za kuwahudumia maelfu ya raia walioathiriwa na mizozo inayolikumba taifa la Sudan Kusini wakiwemo watu 20,000 walio kwenye makao ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa mjini Juba. Jason Nyakundi na taarifa kamili. (Taarifa ya Jason Nayakundi) Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali na yale ya Umoja wa Mataifa yanatoa huduma [...]

23/12/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNICEF yataka watoto Sudan Kusini wapatiwe ulinzi

Kusikiliza / Mlinda amani wa UM akimpatia huduma mtoto kwenye moja ya vituo vya UM huko Juba

Marafiki wote wa Sudan Kusini walio na matumaini makubwa na taifahilochanga, wana hofu kubwa juu ya kile kinachoendelea nchini humo hivi sasa, amesema Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto,UNICEFAnthonyLake. Taarifa hiyo inakuja wakati hali ya mapigano ikiendelea kuripotiwa nchini humo na wananchi wakiwa wamekimbilia kusaka hifadhi kwenye vituo vya Ujumbe [...]

23/12/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNMISS kuimarisha uwepo wake Unity na Jonglei; Ban ataka wanasiasa Sudan Kusini kuchukua hatua

Kusikiliza / Walinda amani wa UNMISS nchini Sudan Kusinin

  Wakati hali ya amani inazidi kuzua sintofahamu huko Sudan Kusini, Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini humo Hilde Johnson ametoa taarifa akithibitisha mipango ya Umoja huo ya kuimarisha uwepo wa vikosi vyake kwenye maeneo ya Bor jimbo la jonglei na Pariang jimbo la Unity. Bi. Johnson amesema azma ya ujumbe [...]

23/12/2013 | Jamii: Habari za wiki, Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930