$209m zahitajika kuwasaidia watu 180,000 walolazimika kuhama Sudan Kusini: OCHA

Kusikiliza /

 

Waathiriwa wa ghasia Sudan Kusini wanaokimbilia ofisi ya UNMISS kutafuta hifadhi

Idadi ya watu wanaoripotiwa kuhama makwao nchini Sudan Kusini tangua kuanza kwa mzozo imepanda na kufikia watu 180, 000 kwa mujibu wa Ofisi ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu katika Umoja wa Mataifa, OCHA. Idadi hiyo inajumuisha pia watu 75,000 ambao wanapewa hifadhi salama kwenye vituo vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa, UNMISS.

Kufikia leo takriban watu 106,000 wamefikiwa na misaada ya aina mbalimbali, nje na ndani ya vituo vya Umoja wa Mataifa. Misaada hiyo ilijumuisha vitu kama chakula, huduma za afya, chanjo, maji safi, huduma za kujisafi na ulinzi.

Kwa mujibu wa OCHA, mashirika ya kutoa misaada yanahitaji hadi dola milioni 209 ili kuitikia mahitaji ya dharura ambayo yamesababishwa na mzozo huo hadi mwezi Machi mwaka 2014.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Oktoba 2017
T N T K J M P
« sep    
 1
2345678
9101112131415
16171819202122
23242526272829
3031