Nyumbani » 19/12/2013 Entries posted on “Disemba 19th, 2013”

Ban asikitishwa na machafuko Sudan Kusini

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa UM, Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, ameelezea kusikitishwa na ripoti zinazoendelea kuibuka za machafuko yanayoendelea kusambaa katika maeneo mengi ya Sudan Kusini, ukiukwaji wa haki za binadamu na mauaji yanayochochewa na chuki za kikabila. Katika taarifa ilotolewa na msemaji wake, Bwana Ban ameitaka serikali na makundi ya upinzani kuheshimu haki za raia na [...]

19/12/2013 | Jamii: Habari za wiki, Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Umoja wa Mataifa waandaa mkakati wa kipaumbele kwa haki za binadamu

Kusikiliza / Naibu Katibu Mkuu wa UM Jan Eliasson

Naibu Katibu Mkuu, Jan Eliasson, amewaambia waandishi wa habari mjini New York kuwa Umoja wa Mataifa umekuwa ukifanya kazi kuandaa mkakati wa kutoa kipaumbele kwa haki za binadamu, ambao utampa kila mmoja msukumo kufanya awezalo kuzuia ukiukwaji wa haki za binadamu, hususan katika mazingira ya migogoro. Bwana Eliasson ametaja mambo matatu muhimu ambayo mkakati huo [...]

19/12/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Ban amteua Han Seung-soo wa Jamhuri ya Korea kuwa mwakilishi wake wa kupunguza maafa.

Kusikiliza / Han Seung-soo

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amemteua Han Seung-soo wa Jamhuri yaKoreakuwa mwakilishi wake maalum wa kupunguza  maafa. Taarifa ilioyotolewa leo alhamisi na ofisi ya msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa imesema mteule huyo akimwakilisha Katibu Mkuu atauganisha ahadi za nchi wanachama, sekta binafsi na asisi za kiraia kuhusu kusaidia kazi [...]

19/12/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Hali Sudan Kusini yaendelea kuwa tete

Kusikiliza / Wahamiaji wanaotafuta hifadhi katika ofisi ya UNMIS kufautia jaribio la kupindua serikali, Sudan kusini

Wakati hali mjini Juba ikiripotiwa kutengamaa, raia wengi bado wanaripotiwa kutafuta hifadhi salama. Kufuatia ripoti ambazo bado hazijathibitishwa za wanfunzi kadhaa kuuawa katika Chuo Kikuu cha Juba, mamia kadhaa ya wanafunzi wengine walosalia kwenye chuo hicho, wameomba kupewa ulinzi kutoka kwa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa Sudan Kusini, UNMISS. Katika eneo jingine mjini Juba liitwalo [...]

19/12/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mwendesha mashtaka ICC aomba kuahirishwa tarehe ya kesi dhidi ya Kenyatta

Kusikiliza / Uhuru Kenyatta, Rais wa Kenya

Mwendesha Mashtaka Mkuu katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita, ICC huko The Hague, Fatou Bensouda leo amewasilisha ombi la kutaka kusogezwa mbele tarehe ya kuanza kusikilizwa kesi dhidi ya Uhuru Kenyatta. Katika ombi hilo, Bensouda anasema kuwa uamuzi wake unazingatia suala la ushahidi kwa mujibu wa mkataba wa Roma. Amesema katika miezi miwili [...]

19/12/2013 | Jamii: Habari za wiki, Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Tushikamane ili tufikie malengo ya milenia kwa pamoja: Rais Baraza Kuu

Kusikiliza / logo

Mshikamano miongoni mwa watu mataifa mbali mbali duniani ni mojawapo ya fursa ya kutokomeza umaskini , amesema Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa John Ashe katika salamu zake za siku ya mshikamano duniani akirejelea lengo la kuanzishwa kwa siku hiyo. Amesema ujumbe wa mwaka huu ni kupunguza tofauti ili kufikia malengo ya maendeleo [...]

19/12/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Baraza Kuu lamkumbuka Nelson Mandela

Kusikiliza / Hayati Nelson Mandela akiwa Umoja wa Mataifa wakati akiwa Rais(1994)

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, leo limefanya kikao maalumu cha kumkumbuka Hayati Nelson Mandela, siku chache baada ya kuzikwa kwake siku ya Jumapili. Joshua Mmali na taarifa kamili (TAARIFA YA JOSHUA) "Tumekusanyika hapa leo kumuenzi mtu ambaye si wa kawaida, Nelson Mandela. Mtu ambaye alitoa msukumo kwa taifa lake, bara na ulimwengu mzima kupitia [...]

19/12/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Utamaduni wa kiarabu washamiri ndani ya siku ya lugha ya kiarabu kwenye UM

Kusikiliza / Suhair Mohammed akimpaka hina mmoja wa washiriki wa maonyesho ya siku ya lugha ya Kiarabu kwenye Umoja wa Mataifa

Lugha ni mojawapo  ya mbinu itumiwayo na binadamu kudhihirisha utamaduni wake. Miongoni mwa lugha zilizovuka mipaka ya nchi na hata bahari ni lugha ya kiarabu ambayo tarehe 18 Disemba ilienziwa ndani ya umoja wa mataifa kwa siku maalum. Tamaduni mbali mbali ziliwekwa bayana kwenye Makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York. Je ni [...]

19/12/2013 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Angalau hakuna mapigano kwa sasa mjini Bangui: UM

Kusikiliza / Raia wakiwa wamesaka hifadhi kwenye uwanja wa ndege Bangui

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa huko Jamhuri ya Afrika ya Kati, Babacar Gaye amezungumzia hali halisi ya usalama nchini humo akielezea kuwa angalau sasa hakuna mapigano mji mkuu Bangui na kwamba kazi ya kupokonya silaha inaendelea. Akizungumza katika mahojiano kwa njia ya simu na Radio ya Umoja wa Mataifa kutoka mjini [...]

19/12/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wanawake wa Syria ni lazima washiriki katika kusaka amani:Brahimi

Kusikiliza / Wanawake nchini Syria wakihama kukimbia mapigano

Mjumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na muungano wa nchi za kiarabu Lakdhar Brahimi amelaani hatua ya kuwafunga na kuwateka nyara wanawake wanaharakati nchiniSyria. Jason Nyakundi na ripoti kamili. (Ripoti ya Jason) Bwana Brahimi amesema kuwaSyriainapitia kipindi kigumu na wanawake wanahitaji kupewa fursa ya kusikilizwa wakati wa mpango wa amani. Akiongea wakati wa kuanza [...]

19/12/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WHO yabainisha maeneo yanayohitaji msaada wa haraka CAR

Kusikiliza / Timu ya wataalamu wa WHO, CAR

Timu ya wataalamu wa shirika la afya ulimwenguni WHO imetembelea kambi moja iliyoko karibu na uwanja wa  ndege wa Mpoko katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, kambi ambayo inahifadhi zaidi ya raia 45,000 waliokimbia machafuko yanayoendelea nchini humo. Wataalamu hao wametembelea eneo hilokwa ajili ya kufanya tathmini juu ya mahitaji muhimu ya kiafya yanayopaswa kutilia [...]

19/12/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wataalamu wa UM watoa ripoti kuhusu Syria na kudai " kulifanyika mipango ya kuwadhuru raia"

Kusikiliza / Wakimbizi wa Syria wanaofurushwa makwao kufuatia mapigano(UNHCR)

Ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyochapishwa leo kuhusiana na uhalifu wa kivita uliofanyika nchini Syria imesema kuwa hakuna shaka kwamba mauwaji ya kupangilika yalifanyika. Ripoti hiyo ambayo ni ya pili kuchapishwa ikiundwa na jopo huru la wataalamu kuhusiana na uvunjifu wa haki za binadamu nchini humo imesema kuwa vikosi vya serikali vilihusika kwa makusudi kuwashambulia [...]

19/12/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kampeni dhidi ya baa la nzige Madagascar yazaa matunda

Kusikiliza / Nzige, Madagascar

Kampeni ya kukabiliana na kuenea kwa tatizo la nzige nchini Madagascar imeanza kuzaa matunda huku juhudi za kutokomeza kabisa tatizo hilo zikiimarishwa. Kufanikiwa kwa kampeni hiyo kulikotishia uhai wa mavuno ya mahindi kutazamia kusadia usalama kwa chakula kwa mamilioni ya raia.Ripoti zaidi na Joseph Msami. (Ripoti ya Msami) Kampeni hiyo iliyotekelezwa kwa ushirikiano wa pamoja [...]

19/12/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031